Mawio Na Machweo
bij 1 winkel
Verwant
Streepjescode: 1230010488027
Alle aanbiedingen
- bol.comMAWIO NA MACHWEONaar de winkel€ 3,73Op voorraad
We verdienen mogelijk commissie als je via deze link koopt. Wat jij betaalt verandert niet.
Over dit product
MAWIO NA MACHWEO Katika familia ya Kumbinanga, mafanikio hupimwa kwa alama za darasani. Kwa Bwana Lameck Kumbinanga, mtoto anayeshindwa kufaulu ni mzigo kwa familia. Mtazamo huu unamfanya Joshua, mtoto wake wa kwanza, kukataliwa, kudharauliwa na kunyimwa upendo anaoutamani kutoka kwa baba yake. Akiwa amevunjwa moyo na kunyanyaswa shuleni, Joshua anakatishwa tamaa na kufanya uamuzi wa kuiba akiba ya wazazi wake na kutoroka nyumbani, akiamini kwamba mbali na familia ndipo atakapoweza kuijenga upya maisha yake. Lakini maisha ya mjini hayana huruma. Joshua anakutana na ukatili wa mitaa, vibarua, kazi ngumu ujira mdogo, umaskini na hatimaye gereza. Katika safari hiyo yenye maumivu, anakutana na Neshikila, mwanamke aliyejeruhiwa na changamoto za maisha. Wawili hao wanajaribu kuunganisha vipande vya maisha yao na kutafuta njia ya kuinuka tena. Wakati huo huo, Joel, mtoto anayesifiwa kwa ufaulu wake, anagundua kuwa kufaulu pekee hakuwezi kumhakikishia maisha aliyoyaota. Familia ya Kumbinanga inaanza kukabili misukosuko inayotikisa misingi yake. Majuto, Mateso ya Nafsi, na Kulaumiana ni sehemu ya maisha ya kila siku katika familia hii. Jua linapozama siku zote Matarajio ni Kuchomoza tena siku inayofuata. MAWIO NA MACHWEO ni simulizi ya kusisimua kuhusu familia, kukataliwa, mapenzi, usaliti, umaskini, matumaini na msamaha. Ni hadithi inayotukumbusha kwamba alama za darasani si kipimo pekee cha thamani ya mwanadamu, wala haziamui mwisho wa safari yake ya maisha.
Omschrijving aangeleverd door bol.com.